Thursday, June 24, 2010

TAMASHA LA AMANI




Mkurugenzi wa YADEN TANZANIA Bw. Franco Longamno akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo leo wakati akitangaza rasmi kufanyika kwa tamasaha la TAEFF Tamasha la utamaduni lijulikanalo kama Tanzania Artist Exchange Forum and Festival ambalo linatarajiwa kufanyika julai 3 kwenye ukumbi wa chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA).
Longamno amesema lengo la kufanya tamasha hilo ni kukutanisha wasanii mbalimbali na kubadilishana uzoefu katika sanaa lakini pia ni kukumbushana juu ya kufanya uchaguzi mkuu wenye amani hapo baadae kwani hata kauli mbiu ya tamasha hilo ni. "HAMASISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU"
Ameongeza kwamba YADEN TANZANIA ina wanachama wapatao 30 duniani kote ambapo vikundi 15 viko Bagamoyo, vikundi 5 viko Dar es salaam, kikundi 1 kiko Moshi, vikundi 2 viko Nairobi na nchini Uholanzi kuna kikundi 1.
Amewaalika wananchi katika tamasha hilo na kuwataka kujitokeza kwa wingi ili waje kujionea mambo mbalimbali katika tamasha hilo kubwa ambalo halitakuwa na kiingilio chochote yaani liitakuwa ni bure kabisa, mgeni rasmi katika tamasha hilo ni mbunge wa Bagamoyo Mh. Dr. Shukuru Kawambwa, katika picha kushoto ni Afisa habari Mwandamizi Idara ya Habari Maelezo Benjamin Sawe..



No comments:

Post a Comment