Friday, December 25, 2009

MSONDO KUINGIA MTWARA



BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini Msondo Music bandi watafanya zihara ya utambulisho wa albam yao mpya ya huna shukrani i ambapo Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' ameliambia gazeti hili kwamba Bendi hiyo kwa sasa ipo mikoa ya kusini kuwapa wapenzi burudani za x masi na kutakiana heri ya mwaka mpyaAlisema katika utambulisho huo kwa mashabiki wa Msondo pia watapata nyimbo mpya kabisa zilizotungwa kwa ajiri ya albam ya mwaka 2010
Wanamuziki wa bendi ya msondo ngoma wakiwajibika wakati wa moja ya maonesho yao ni Roman Mn'gande Romario na Hamisi Mnyupe.(Picha na Rajabu Mhamila)

Akielezea maandalizi zaidi Mhamila alisema licha ya kutambulisha albam bendi hiyo pia wamejipanga kutoa zawadi kwa mashabiki wao, ambapo albam yao mpya,iliyoingia sokoni hivi kalibuni kuuzwa mtaani pia wameombwa kununuwa albam hiyo wapate kusikiliza majumbani mwao kwa ajiri ya sikukuu katika ziara hiyo ya utambulisho wa albamu siku ya alhamisi watakuwa Lindi katika ukumbi wa Comit Center, ijumaa Mtwara watapiga katika ukumbi wa Jakaya aidha jumamosi watapiga Masasi katika ukumbi maarufu na jumamosi watakuwa nachingwea katika ukumbi wa nachngwea pub, katika mkesha wa mwaka mpya watakuwa Rwangwa
Alisema nyimbo zitakazotambulishwa katika dhihara hiyo ni pamoja na wimbo uliobeba albam hiyo, Huna shukrani uliotungwa na Saidi Mabera,Kiapo (husein jumbe) aki yangu ipo wapi (Uluka Uvuluge) Mama Cos, uliotungwa na marehemu (Josephe Maina) Albino (Juma Katundu) Machimbo Isihaka Kitima dj papa upanga) na Cheo ni Dhamana (Eddo Sanga)
Aidha aliwataja wanenguaji watakaokuwa wanatoa burudani katika safu hiyo kuwa ni Amina Said 'quen Emmy' Nacho Mpendu 'mama Nzawisa' na Amiri Saidi 'Dongo' aidha rapa wa bendi hiyo Romani Mng'ande 'Romario' atawachenguwa mashabiki watakaofika katika onesho hilo wakiongonzwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Muhidini Gurumo,na kiongozi wa bendi hiyo Saidi Mabela

No comments:

Post a Comment