Thursday, August 26, 2010

Rock City Marathon 2010’ yatafanyika Septemba 26 mwaka huu Jijini Mwanza.



Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui (kushoto)
akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa
mashindano ya riadha yanayojulikana kama Rock City Marathon yanayotarajiwa
kufanyika Mwanza Septemba 26 mwaka huu.Katikati ni Mratibu wa mashindano hayo
kutoka Kampuni ya Capital Plus Ltd ambao ndio waandaaji Raymond Kanyambo na
kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Amant Macha
aliyekuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam





KAMPUNI ya Capital-Plus International (CPI) imeandaa mashindano ya riadha ya kilomita 21 yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2010’ yatakayofanyika Septemba 26 mwaka huu Jijini Mwanza.
Tunafanya mashindano haya kwa mara ya pili ambapo ya kwanza yalifanyika mwaka jana na kwamba tunatarajia mbio hizo zitaanzia uwanja wa CCM Kirumba kuelekea njia tofauti za Jiji la Mwanza na kumalizia katika uwanja huo.
Kama ilivyokuwa katika mashindano yaliyopita tunatarajia wanariadha kutoka sehemu mbalimbali mchini pamoja na nchi jirani watashiriki katika mashindano hayo ya aina yake katika ukanda huo wa Ziwa.
Mialiko kwa ajili ya ushiriki itatumwa baada ya kutoa tarifa hizi kupitia vyama vya michezo husika ambavyo ni Jamhuri ya watu wa Congo (DRC), Rwanda, Burundi, Kenya,Uganda na Zambia.
Mashindano haya pamoja na mbio hizo ndefu pia yatahusisha matukio mengine kadhaa ambayo ni mbio za kilomita 5 kwa wote , mbio za kilomita 3 kwa wazee wa kati ya umri wa miaka 55 na zaidi, mbio za kilomita 3 kwa watu wenye ulemavu na mbio za kilomita 2 kwa watoto wa kati ya umri wa miaka 7 -10.
Ada za ushiriki kwa mashindano haya ni sh. 500/= kwa mbio ndefu za kilomita 21, sh.300/= mbio za kilomita 5 na 3 wakati mbio zitakazohusisha watoto ni bure.
Tumeamua kupanua wigo wa ushiriki mwaka huu kutokana na kutambua umuhimu wa michezo kwa rika mbalimnbali lakini muhimu zaidi ni mapendekezo tofauti tuliyopokea kupitia wadau mbalimbali baada ya kumalizika kwa mashindano ya mwaka jana.
Mashindano haya yamedhaminiwa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL),Mfuko wa Pensheni wa Taifa (PPF), Hoteli ya New Africa, NSSF Clouds FM na Isamilo Lodge ya Mwanza.
Fomu kwa ajili ya kujisajili zinapatikana Isamilo Lodge Mwanza, Ofisi za uwanja wa CCM Kirumba, Ofisi za Capital- Plus International Limited- DSM, Makao Makuu ya Chama cha Riadha Tanzania (RT) Dar es Salaama, Ofisi za RT Mwanza. Pia washiriki wanaweza kupata fomu hiyo katika www.capitalplus.co.tz / rockcitymarathon.com
Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi kuhusiana na mashindano haya unaweza kutuandikia kupitia info@capitalplus.co.tz.




 

No comments:

Post a Comment