Tuesday, April 5, 2011

SABA WAONGEZWA U 23



Afisa habari wa shirikisho la soka la kandanda akitaja walongezwa katika timu ya taifa itakayocheza dhidi ya cameroun


Kocha Jamhuri Kihwelo ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi chake cha U23 kwa
ajili ya mechi ya marudiano ya mchujo ya michuano ya Olimpiki dhidi ya Cameroon
itakayochezwa Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni Kigi Makasi kutoka Yanga, David Luhende (Kagera Sugar), Jabir
Aziz (Azam), Kelvin Chale (Simba), Ali Lundenga (Kagera Sugar), Mrisho Ngasa
(Azam) na Juma Abdul (Mtibwa Sugar).
VIINGILIO U23 v CAMEROON
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni kuanzia sh.
1,000. Mashabiki watakaokaa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa (orange)
ndiyo watakaolipa kiasi hicho wakati VIP B na VIP C kiingilio kitakuwa sh.
5,000. Jukwaa la VIP A lenye viti 745 kiingilio kitakuwa sh. 10,000. Tiketi
zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mechi.
Tiketi zitauzwa katika vituo vya OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora/Ohio, Bigbon Msimbazi (Kariakoo)
na Uwanja wa Uhuru. Mechi itaanza saa 10 kamili. Cameroon imewasili nchini jana
saa 5.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ikiwa na wachezaji 23 na imefikia
Paradise City Hotel.
Mwamuzi wa mechi hiyo ni Aime Ndayisenga akisaidiwa na Desire Gahungu,
Jean-Claude Birumushahu na Athanase Niyongabo, wote kutoka Burundi. Kamishna wa
mchezo huo ni Charles Masembe kutoka Uganda.
FIFA YAISIMAMISHA BOSNIA-HERZEGOVINA
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) limeisimamisha
Bosnia-Herzegovina kuanzia Aprili Mosi mwaka huu baada ya Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchi hiyo (FFBH) kutopitisha Katiba yake
iliyofanyiwa marekebisho kwa kuzingatia matakwa ya FIFA na Shirikisho la Mpira
wa Miguu la Ulaya (UEFA).

Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke iliyotumwa kwa
wanachama wake, FFBH inapoteza haki zote ilizokuwa nazo kutokana na uanachama
wake kwa Shirikisho hilo hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine.
Kutokana na kusimamishwa huko, wanachama wote wa FIFA hawatakiwi kushirikiana na
FF BH katika masuala yoyote isipokuwa yale yanayohusu mchezaji binafsi. Hatua
hiyo imefikiwa kutoka na uamuzi uliofikiwa Oktoba 28 mwaka jana na Kamati ya
Utendaji ya FIFA kuwa FFBH iwe imetekeleza matakwa hayo kufikia Machi 31 mwaka
huu.

No comments:

Post a Comment