Monday, February 22, 2010

kameongezewa muda


Manchester City itampatia mshambuliaji wake Carlos Tevez muda zaidi atakaohitaji kumhudumia binti yake aliyezaliwa kabla ya muda.
Tevez, hadi sasa hajacheza michezo mitatu na timu yake, baada ya kupewa likizo ya udhuru kwenda Argentina ambapo binti yake aitwaye, Katie, yupo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum.
Maofisa wa klabu ya Manchester City wanasema walizungumza na Tevez lakini hawafahamu ni lini atarejea.
Timu hiyo chini ya Roberto Mancini itakabiliana na Stoke siku ya Jumatano katika mfululizo wa michezo ya Kombe la FA na siku ya Jumamosi katika Ligi Kuu ya Soka ya England watakwaruzana na Chelsea.

No comments:

Post a Comment