Wednesday, October 20, 2010

NI UBINIFU WA MAVAZI DAR


Swahili Fashion Week 2010 kwa mwaka wa tatu yazinduliwa rasmi

Wabunifu wa mavazi 24 kuonyesha kwa kipindi ch siku tatu mfululizo

Kwa mara ya kwanza kutakuwa na maonesho ya bidhaa mbalimbali

Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week itafanyika Karimjee Hall kuanzi tarehe 4 hadi 6 November 2010, Dar Es Salaam , Tanzania .

Swahili Fashion Week itawaleta pamoja wabunifu wa mavazi 24 kutoka nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili ili kuweza kuonyesha ubunifu wao katika kubuni mavazi ya aina mbalimbali kwa kutumia aina mbalimbali za malighafi.

Wabunifu watakaoonesha mavazi katika Swahili Fashion Week kwa mwaka huu ni pamoja na Ailinda Sawe, Manju Msita, Kemi Kalikawe, Christine Mhando, Shellina Ibrahim, Farha Naaz Sultan, Gabriel Mollel, Robi Morro, Asia Idarous, Zamda George, Khadija Mwanamboka, Jamilla Vera Swai and Made by Afrika. wabunifu kutoka Kenya ni Sonu Sharma, Moo Cow, KiKoromeo, John Kavike na Kooroo, na kutoka Uganda ni mbunifu Stella Atal.


“Pamoja na maonyesho ya mavazi, mwaka huu Swahili Fashion Week itakwenda sambamba na tamasha la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zenye asili ya mswahili kutoka mwambao wa Afrika mashariki”. Alisema Mustafa Hassanali muaandaaji y tukio la Swahili Fashion Week.


“Tunafungua milango zaidi kwa ajili ya watazamaji wapya wa Swahili Fashion Week, amboa watapata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali. Tamasha hili ambalo linazileta pamoja bidhaa mbalimbali za sanaa na utamaduni wa mswahili, pia litahamasisha ubunifu zaidi katika bidhaa zinazokwenda sambamba na maisha halisi ya jamii ya watu wanaoongea lugha ya Kiswahili kwa kukutana pamoja na kubadilisha mawazo na kujifunza uzoefu mpya katika masuala yanayohusiana na sanaa kwa ujumla.” Aliaongeza Hassanali.


Pamoja na maonyesho, pia kutakuwepo aina tofauti za burudani kutoka kwa vikundi

Mbalimbali vya muziki, uchoraji wa hina, usukaji mikeka, sambamba na semina za aina tofauti zitakazo washirikisha wabunifu wa mavazi.

Aidha Swahili fashion Week imeandaa aina tofauti za zawadi zitakazotolewa mwaka huu kwa lengo la kutambua na kuthamini vipaji vya aina mbalimbali vitakavyooneshwa, ikiwa ni pamoja na zawadi ya mwaka kwa mbunifu anaechipukia.

Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na Home of Swahili Fashion week Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, EATV, East Africa Radio, Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery LTD, 1 & 1 internet solutions, Sengi Tours, Ifashion na 361 Degrees.



Taarifa kwa Wahariri

Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.

Swahili fashion week in tukio ambalo linawajumuisha wabunifu wakongwe na wale wanaochipukia kuonyesha kazi zao, pia kutoa nafasi kwa wapenzi wote wa sanaa ya mavazi kujumuika pamoja na kufurahia ubunifu wa watanzania na kutoka nchi za jirani.

“Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kuwa sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa na kwa nchi za Afrika Mahariki”. Alifafanua Mustafa Muanzilishi na Muuandaaji wa Swahili Fashion Week.








No comments:

Post a Comment