Tuesday, November 3, 2009

ZIARA YA RAS NAS HUKO OSLO

Ile ziara ya mwanamuziki Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi katika miji sita ya Norway karibu inamalizika. Hapa ni kwenye ukumbi wa MS Innvik, Oslo, ambapo Ras Nas na kikosi chake waliwasha moto mkali usiku wa Halloween; Jumamosi iliyopita. Hivi sasa Ras Nas amejipanga kufyatua CD ya muziki na mashairi "Double Focus". Mashairi yanatoka kwenye kitabu ambacho Nasibu aliandika mwaka 1989 pamoja na shairi moja la Shabaan Roberts “Titi la Mama”. Kwa hiyo hivi sasa kaa chonjo!
Wadau,
Kongoi Productions

No comments:

Post a Comment