Thursday, January 28, 2010

zain yaja na huduma mpya


Meneja Masoko wa Zain Kelvin Twisa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski juu ya faida watakazozipata wateja wa kampuni hiyo katika ofa mpya ya Nipe Nikupe wenginer katika picha kutoka kushoto ni Group Manager Steve Torade,Managing Director Khaled Muhtadi,pamoja na Ahsan Syed.
Wateja wa Zain Tanzania nchi nzima sasa watarudishiwa papo kwa papo pesa yoyote watakayotumia kuzungumza kwenye simu zao zao mkononi kupitia ofa kabambe ya Nipe Nikupe.
Zain, kampuni inayoheshimika zaidi nchini Tanzania imethibitisha leo kwamba mteja wa Zain atarudishiwa shilingi 200 papo kwa papo kwa kila shilingi 200 atakayotumia kuzungumza kila siku. Hii inamaanisha kwamba kila shilingi 200 inayotumika kuzungumza kwenye mtandao wa Zain inakurudishia kiashi hicho hicho ili uweze kuendelea kuzungumza kwenye mtandao wa Zain.
inamrudishia teja akitumia shilingi 200 kwenye simu ya kutoka mtandao wa Zain kwenda Zain atarudishiwa kiasi hicho cha pesa ili akitumie kwenye mtandao mwingine. Ofa hii sio kwa simu zinazopigwa kutoka mtandao wa Zain kwenda Zain tu, bali hata zile zinazopigwa kutoka Zain kwenda kwenye mtandao mwingine wowote ule nchini. Kwa kila 200 utakayotumia kupiga simu kwenda kwenye mtandao mwingine, utarudishiwa kiasi hicho hicho papo papo ili uendelee kupiga simu kwenda kwenye miandao mwingine.
Ofa hii kabambe ni ya kwanza ya aina yake nchini Tanzania na inaweka historia katika sekta ya mawasiliano nchini na kudhihirisha hatua zinazochukuliwa na Zain kuongoza nchini katika kuanzisha mawasiliano ya gharama nafuu kati ya mitandao ya simu za mkononi.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Nipe Nikupe Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khaled Muhtadi alisema kuanzia leo wateja wote wa Zain walio katika mpango wa Malipo Kabla watakao jisajili katika mpango huu watarudishiwa muda wa maongezi waliotumia papo papo na wanaweza kuutumia kupiga simu za kwenda mtandao wa Zain au mtandao wowote mwingine ule nchini.
Ofa ya Nipe Nikupe itaendelea kutoa fursa kwa wateja wa Zain wanaohitaji kuwasiliana na ndugu na familia au kufanikisha mahitaji yao ya biashara nchini kote kunufaika na mtandao mpana wa Zain ulioenea maeneo mengi zaidi nchi kuliko mtandao mwingine wowote pamoja na bidhaa za ubunifu wa hali ya juu. Wateja wa Zain wataweza kutumia bonasi walizopata kupiga simu kwenda Zain au mtandao mwingine wowote siku hiyo hiyo kabla muda wa bonsai haujaisha saa sita usiku.
Kujisajili katika Nipe Nikupe mteja wa Zain anapaswa kutuma SMS ya neno NIPE mara moja tu kwenda 15444 na ujumbe huo utagharimu Tshs 500 tu ambayo itatozwa mara moja tu.



picha na fuulshangwe

No comments:

Post a Comment