Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaal Afande Suleiman Kova leo ameongea na waandishi wa habari na kutoa taarifa juu ya sakata la mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Utangazaji Tanzania (TBC) juu ya madai ya kupokea rushwa ya shilingi milioni 10 kutoka kwa bw. Maiko Calos aliyekuwa mhasibu wa Harmashauri ya Mji wa Bagamoyo kabla ya kutemeshwa mzigo na Waziri mkuu Mizengo pinda hivi karibuni.
Afande kova akizungumzaia sakata hilo amesema Bwana Maiko Calos alitoa taarifa polisi akidai kuna watu wanamsumbu sana na kumtisha wakidai awape shilingi milioni 10 kabla ya kuibua kashfa zake kwenye vyombo vya habari, hivyo Afande kova aliwaamuru vijana wake kufuatilia tukio hilo katika mgahawa wa City Garden jijini Dar es alaam na kuikuta gari ikiwa imeegeshwa , ilibidi Maiko awasiliane na huyo mtu ili waingie hapo hotelini hata hivyo mtu huyo alikataa hivyo wakamfuata kwenye gari na kukuta Ni jerry Murro mwandishi wa TBC.
Anasema walimchukua mpaka kituo cha polisi na kuchukua maelezo ya bwana Maiko ambaye alisema anamfahamu Jerry Murro kwani wamekuwa wakikutana katika maeneo kadhaa jijini, pia akadai kwamba kuna miwani yake aliisahau kwenye gari ya Jerry Murro na pia kuna pingu na Silaha yaani bastola ambvyo mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia kumtishia ili atoe hizo fedha.
Hata hivyo afande Sulaiman Kova hakuthibitisha kwamba Jerry Murro amekamatwa na hizo shilingi milioni 10, lakini amesema kujipati fedha au kumdai fedha mtu yeyote kwa kumtishia ni kosa la jinai, hivyo kutokana na mazingira ya maelezo ya mlalamikaji na vielelezo vinatufanya kuamini kwamba tukio hilo lilikuwepo, ameongeza kuwa hawakuweza kuwashirikisha (PCCB) Kikosi cha kuzuia Rushwa katika mtego huo kwakuwa muda ulikuwa ni mdogo na mtuhumiwa angeweza kukimbia na kuwapotea
Kuhusu Bastola ambayo inamilikiwa na Jerry Murro Afande Kova amesema silaha hiyo imetengenezwa nchini Chec. Repumlic ni SZ 97 B NO A 6466 inayobeba risasi 10 anaimiliki kihalali kabisa, ina vibali vyote na alipewa kwa ajili ya kujilinda na maadui zake kutokana na kazi zake za habari za uchunguzi, Isipokuwa pingu ambazo hakuna raia ambaye anaruhusiwa kumiliki kisheria
Ameongeza kwamba Kesi hiyo wataipeleka kwa mwanasheria wa Serikali ili aone kama kuna kesi ya kujibu na kuipeleka mahakamani ili haki itendeke kwa kila upande na kama itakuwa vinginevyo watamuita bwana Maiko Calos ambaye ni mlalamikaji na kumwambia yaliyojiri kutoka kwa mwanasheria wa Serikali
No comments:
Post a Comment