Friday, September 17, 2010

HIVI Steven Delano Smith alivyohamasisha kikapu Tanzania



STEVEN DELANO SMITH akitoa maelekezo ya kucheza mpira wakikapu katika viwanja vya leaders club hii leo amekuja kuhamamsisha mpira huo nchi vilevile aliwahi kucheza timu moja na michael jordan

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania TBF tunapenda kutoa shukrani zetu kwa Coca Cola kupitia kinywaji chake cha Sprite ambapo leo hii kwa mara nyingine kwa kushirikiana na TBF vijana wetu chini ya miaka 18 wanaendelea kupata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali za kimchezo na kusaidia kuamsha hamasa katika mchezo wa Mpira wa kikapu nchini.

Ujio wa Steven Smith ni chachu kwa vijana wetu na tunategemea katika clinic hii tutakuwa tumejifunza mambo mengi hasa kwa makocha wetu ambao wamepata nafasi ya kushiriki ni sehemu ya pekee ya kuboresha yale waliyo nayo katika ufundishaji.



hapa vijana wanajenga stamina ya kukaba wakiwa kiwanjani.


TBF inapenda kuwahakikishia Coca cola kuwa itatoa ushirikiano wa karibu sana katika kuakikisha mchezo wa Mpira wa Kikapu unakuja na sura mpya, tunashukuru tumeanza katika kulea vipaji lakini pamoja na hilo wote tunapajua hapa tulipo kiwanja cha Leaders hakikua katika hali hii lakini leo Sprite wametuongezea mahali ambapo vijana wetu watapata nafasi ya kucheza bila kwenda umbali mrefu,na huu ni mwanzo tunamatumaini vingine vinafuata.

Changamoto pekee ambayo tunayo kwasasa ni kuakikisha tunapata viwanja vingi Tanzania, ili kutoa fursa kwa vijana kucheza, lakini pia kupata walimu wa kutosha wa kuwafundisha vijana hawa, tunapenda kutoa wito kwa makocha kushiriki kozi za ukocha mara zinapotangazwa lakini pia tunaomba Kampuni ya Cocacola kupitia kinywaji cha Sprite watusaidie kutekeleza haya na pia kutuletea makocha wenye viwango vya juu ili wapate kutoa mafunzo kama haya kwa makocha wetu.



Marty Conlon akimwelekeza kijana jinsi ya kujenga stamina na kukabiliana na adui.

Pia tunatoa wito kwa makampuni mengine ndani na nje ya nchi kuiga mfano huu wa Cocacola na kujitokeza kudhamini michezo na kuwekeza katika kukuza vijana na hii itasidia kuongeza soko la bidhaa kama ambavyo makampuni yanayowekeza na kudhamini michezo yalivyofanikiwa.

Tunatoa shukrani nyingi kwa Rais Jakaya Kikwete, Mlezi wetu Jaji Mkuu Agustono Ramadhani, Hasheem Thabeet, Waziri Mkuchuka na Naibu Waziri Joel Bendera na Viongozi wote wa Wizara ya Michezo, Baraza la Michezo la Taifa na viongozi wote wa Serikali ya jumhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikano mzuri wanaotupatia. Sisi tunaahidi tutaendelea kushirikiana nao katika kuhakisha tunatekeleza ahadi na mikakati yetu ya kuendeleza vijana kupitia mchezo huu unaokuwa kwa kasi nchini wa kikapu.


Tunapenda kueleza furaha yetu kwa ushirikiano mzuri kutoa katika Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,yapo mambo mengi yamesha fanyika katika kutafuta makocha watakao lea hivi vipaji na tunategemea kupata program kama hizo katika siku zijazo.

TBF inachukua nafasi hii kukukaribisha Steven Smith, Marty Conlon na wadau wengine wote mliokuja nchini Tanzania, tunategemea na mtajifunza mambo mazuri ya nchi yetu pamoja na ukarimu wa Tanzania karibuni sana.



No comments:

Post a Comment