Wednesday, May 26, 2010

BILIONI 7 US DOLLARS KUTUMIKA!!(GAS NA MAFUTA).

Katikati Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania Mh.William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba na Kampuni ya TPDC,Ophir Energy wakishirikiana na BG Group wa utafutaji na uendelezaji wa Gas na Mafuta nchini Tanzania,(Kulia) Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw.David Jairo,(Kushoto) Mwakilishi wa kampuni ya Ophir Energy(Techinical Director) Bw.Jonathan Taylor.
Na Mwandishi wetu.
Wizara ya Nishati na Madini leo imeasini mkataba wa kihistoria wa mikakati ya utafutaji na uendelezaji wa gesi na mafuta hapa nchini ambao serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiwakilishwa na Waziri wa Nishati na Madini,wamesaini maktaba na kampuni ya TPDC and Ophir Energy wakishirikiana na BG Group.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam Waziri wa Nishati na Madini Mh.William Mganga Ngeleja amesema kwa mara nyingine historia ya utafutaji wa gesi na mafuta huu ni wa kihistoria kwa sababu TPDC wamesaini mkataba kama mtu mmoja katika utafutaji wa Gas na Mafuta.
Aidha Waziri Ngeleja amesema zaidi ya shilingi bilioni 7 US Dollars zinawekezwa katika mradi huo na TPDC wakishirikiana na Ophir Energy pamoja na BG Group ambapo utafutaji wa Gas huu na hatimaye mafuta utazingatia mahitaji ya mtanzania kwa ujumla kwa kuhakikisha kuwa Gas itakayopatikana au kuzalishwa itatumika kwa ajili ya kutuwezesha kujenga viwanda vya mbolea ili kuboresha kilimo hapa nchini,kutupa uwezo wa kuzalisha umeme wa zaidi,kuhumia viwanda vya cement vitakavyotusaidia kupata macementors watakaowekeza kwa wingi hapa nchini ambapo uwekezaji huo utasaidia kwa kiwango cha juu sana katika maendeleo ya mtanzania.
Akihitimisha Waziri Ngeleja amesema nchi za jumuiya ya madola zinakitengo cha washauri ambazo huchangia kujadili matatizo mbalimbali ya wanachama wake,Tanzania sasa ni wanachama katika pande mbili za mashariki na kati.
Kwa upande wake Mwakilishi wa kampuni ya Ophir Energy ,Technical Director Bw. Jonathan Taylor amesema mkataba huu utawawezesha baadhi ya Watanzania kupata ajira wakati wa uandaaji wa ujenzi wa plant.
Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu faida za mradi huo alisema si rahisi kwa hivi sasa kujua mradi utakuwa na faida gani katika nchi ya Tanzania kwani ni mapema sana na hivyo akawataka Watanzania kuangalia baada ya miaka 10 nini kitakuwepo katika mradi huo na faida zitaonekana.

Waziri wa Nishati na Madini Mh.William Ngeleja(kulia) na Mwakilishi wa Ophir Energy Bw.Jonathan Taylor(kushoto) wakisaini mikataba ya utafutaji na uendeshaji wa Gas na Mafuta nchini Tanzania wenye thamani ya shilingi Bilioni 7 US dollars,Nyuma yao ni Mh.Nimrod E. Mkono Mbunge wa Musoma Vijijini akiwa na wanasheria wakati wa kusaini mikataba hiyo.


No comments:

Post a Comment