Friday, May 28, 2010

liyumba akataa rufaa


Globu ya Jamii
Zikiwa zimepita siku nne baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumhukumu kifungo cha miaka miwili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba, mawakili wanaomtetea wameibuka na kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.Rufani hiyo imekatwa leo katika mahakama ya rufani Tanzania na mawakili wa upende wa utetezi wanaomtetea Liyumba.Liyumba ambaye anawakilishwa na mawakili Hilary Mkate, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu na Onesmo Kiyauke amekata rufani hiyo ambayo imepewa namba 56/2010 ambapo ndani yake amegusia sababu 12 zilizompelekea kufikia uamuzi huo wa ukataji rufani.Katika sababu ya kwanza Liyumba alidai kuwa jopo la mahakimu linaloundwa na mahakimu watatu, ambalo lilikuwa likiskiliza kesi yake, lilishindwa kuchambua vyema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo jambo lililopelekea kutoafautiana wakati wa usomwaji wa hukumu.Sababu nyingine aliyotoa Liyumba ni kuwa mahakimu wawili kati ya watatu waliopo katika jopo la mahakimu lililokuwa likisikiliza kesi yake, ambao walimkuta na hatia walikosea kutokubali kuwa mabadiliko ya ujenzi wa majengo pacha ya BoT yalikuwa yakifanywa na timu ya wataalamu wa ujenzi kwa ushirikiano wa aliyekuwa Meneja Miradi wa BoT bwana Deogratius Kweka.Pia katika sababu nyingine ameshindwa kukubaliana na mahakama ya Kisutu kwa kushindwa kukubaliana kuwa Meneja Miradi wa benki yaani Kweka ndiye aliyekuwa akihusika na mradi huo ambapo aliongeza kuwa ndiye aliyekuwa akiwajibika kwa aliyekuwa gavana wa Benki hiyo ambaye sasa ni Marehemu, marehemu Daud Balali.Aidha Liyumba alipinga hukumu ya kifungo iliyotolewa na mahakimu hao kwa madai kuwa walifanya makosa kutupa ushahidi wote wa utetezi alioutoa mahakani hapo akiwa na shahidi wake ambaye ni aliyekuwa Kaimu Katibu wa BoT Bosco Kimela, kwa kile mahakama ilichodai kuwa wote walikuwa wakiishi rumande kutokana na kuwa na tuhuma mbali mbali.Kwa upande wa sababu hiyo pia, Liyumba alidai kuwa mahakama hiyo ilikosea kusema kuwa ushahidi wao wa utetezi ulikuwa ni wa kutunga , na kuongeza kuwa yeye hakubaliani na hilo kwani ushahidi walioutoa ulikuwa ni wa kweli na si kama ambavyo mahakama inadai.Mbali na hilo, Liyumba katika sababu nyingine alipinga uamuzi wa mahakimu hao wawili uliodai kuwa malipo ya kufanyika kwa mabadiliko ya ujenzi wa jengo la BoT, aliyafanya yeye kwani hakuna ushahidi ulioko kwenye kumbukumbu za mahakama unaoenesha hilo, na kwamba anashangaa mahakama imeutoa wapi ushahidi huo.Katika sababu nyingine, Liyumba alidai kuwa mahakama haikuwa sahihi kusema kuwa uhidhinishaji wa kufanyika kwa matumizi ya utekelezaji kabla ya, kufanyika kwa jambo si sahihi kwani taratibu za fedha za BoT za mwaka 2006 zinaruhusu kufanyika hilo.Pia Liyumba alidai katika hati ya rufani hiyo kuwa mahakama ya Kisutu, ilikosea kusema kuwa hakuwa na mamlaka ya kusahini barua za benki kuu, na kuongeza kuwa jambo hilo si la kweni kwasababu yeye akiwa kama Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa benki hiyo, alikuwa na mamlaka ya kusahini barua za kibenki.Aidha Liyumba amepinga kile kilichosemwa na mahakimu wa mahakama hiyo, kwamba upande wa mashtaka umeweza kuthibisha kesi hiyo kupitia ushahidi wake pasipokuwapo na dosari, na kwamba hilo si la kweli kwani kuna mashaka mengi yaliyopo ndani ya ushahidi wa upande huo.Katika sababu ya mwisho Liyumba alidai kwamba, wakati wa kusomwa kwa hukumu dhidi yake mahakama ya Kisutu ilikosea kwa kushindwa kufuata taratibu zilizoahinishwa kwa mujibu wa sheria.Rufani hiyo bado haijapangiwa Jaji wa kuisikiliza ikiwa ni pamoja na tarehe ya kusikilizwa kwake.Hivi karibuni mahakama ya Kisutu ilimhukumu Liyumba kifungo cha miaka 2 gerezani, baada ya kuonekana kuwa ana hatia dhidi ya tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake iliyokuwa ikimkabili.Hata hivyo jopo linaloundwa na mahakimu watatu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo, lishindwa kuafikiana wakati wa kutoa hukumu hiyo jambo lilosababisha kuwapo kwa hukumu mbili tofauti, huku ukumu iliyoungwa mkono na Mahakimu wawili ikimfunga Liyumba.Wakati hukumu hiyo iliyoandaliwa na Hakimu Benedict Mwangwa pamoja na Hakimu Lameck Mlacha ikimfunga Liyumba, mambo yalikuwa tofauti kwa Hakimu Edson Mkasimongwa ambaye aliaandaa hukumu iliyotaka Liyumba aachiwe huru kwa kile alichokisema kuwa hakuwa na hatia.Lakini kutokana na hukumu ya kumkuta na hatia Liyumba kuungwa mkono na Hakimu zaidi ya mmoja, ilipelekea mahakama hiyo kuichukulia hukumu hiyo kama utekelezaji wa mahakama, huku hukumu ya kuachiwa huru yaani iliyoandaliwa na Mkasimongwa ikisomwa na kubakia kama kumbu kumbu za mahakama katika kesi hiyo.Katika hukumu ya mahakimu wawili iliyomfunga Liyumba, Mahakimu haoa walisema kuwa ushahidi wa mashahidi nane kutoka upande wa mashtaka uliifanya mahakama hiyo kuamini kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo hasa kwa kujipa madaraka ya kusahini baraua za uhidhinishaji wa kufanyika kwa mabadiliko ya ujenzi wa majengo ya BoT pasipo kuwapo na mamlaka ya kufanya hivyo.Kwa upande wa Mkasimongwa, yeye alisema kuwa mahakama imuachie huru Liyumba kwasababu upande wa mashataka haukuweza kuithibitishia mahakama kesi hiyo na kwamba kuhusiana na hoja ya kuwa na mamlaka, Liyumba alikuwa na mamlaka ya kusahini barua hizo za kibenki.

michuzi.blogspot under stand

No comments:

Post a Comment