Thursday, August 27, 2009

SERIKALI YAKANUSHA KUUZWA KWA TBC


Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania kupitia kwa waziri wa Habari utamaduni na Michezo Kapteni mstaafu George H Mkuchika (MB)
amekanusha vikali taarifa zilizo tolewa na Gazeti la Mwanahalisi la tarehe 26 agosti, 2009 katika toleo la 151 kuwa serikali imetuhumiwa kuuza kinyemera shirika la utangazaji tanzania tuhuma hizo zimetokana baada ya shirika hilo kuunda kampuni iitwayo star media Tanzania limited kwa ubia na mwekezaji aliyeteuliwa kihalali ilikutekeleza kuiwezesha TBC kutangaza matangazo kwa mfumo wa Digital television multiplex services. kwa maana hiyo siyo sahihi kusema Tbc imeuzwa kutokana na ubia huo TBC sasa itachangia asilimia 35 kutokana na rasilimali zake na sio fedha na mwekezaji kutoka china M/S atachangia asilimia 65
serikali inazidi kusisitiza kwamba vyombo vya habarikuzingatia weledi wa taaluma ya habari na kuandika habari zenye ukweli bila kupotosha umma


No comments:

Post a Comment