Wednesday, September 2, 2009

JAKAYA KUINUA KIKAPU MWEZI OKTOBA

Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) linawataarifu wadau na wapenzi wa mpira kikapu kuwa limeandaa siku ya mchezo wa kikapu wa hisani (Basketball Charity Day) kuchangia maendeleo ya mchezo huu nchini siku hiii itakuwa jumamosi tarehe 24 october hapa katika uwanja wa ndani wa taifa,Dar es salaam.
Katika siku hiyo wadau na wapenzi wa mchezo wa mpira wakiwemo wachezaji wa zamani viongozi mbalimbali wa serikali na mashirika, mabalozi na watanzania wote wenye mapenzi mema na mpira wa kikapu watajumuika pamoja kucheza michezo ya hisani katika kuenzi na kuchangia maendeleo huu hapa Tanzania.
Mgeni rasmi katika tamasha hili anatarajiwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh DR jakaya Mrisho kikwete ambaye pia atakuwa mshiriki .pamoja naye watakuwepo viongozi wengine wakiwemo jaji mkuu Mh Augustino Ramadhani spika wa bunge Mh Samwel sita pamoja na mawaziri ,mabarozi na viongozi wengine wa mashirika na makampuni mbalimbali nchini.
Shirikisho la mpira wa kikapu linawaomba wadau ikiwemo watu binafsi ,mashirika,balozi mbalmbali na serikali kujitokeza kuchangia maendeleo ya mpira wa kikapu ili tuweze kujenga na kupata wachezaji wengi zaidi katika anga ya kimataifa .
(TBF) imeendaa kadi maalum ambazo wale watakaopenda kushiriki kucheza au kuangalia michezo ya hiyo katika siku hiyo watazipata katika kutafuta wafadhiri watakao dhamini kwenye ushirika wao(wa kucheza au kuangalia )na fedha zitakazo patikana zitawasilishwa TBF Kutekeleza lengo lililokusudiwa.
Kwa maelezo zaidi na kupata kadi hizi,wadau na wapenzi wa mpira wa kikapu wanaombwa kuwasalimia na Katibu wa mkuu TBF bwana Lawrence Cheyo kwa nambari za simu 0754 272065/0713272065

No comments:

Post a Comment