Monday, August 30, 2010

TUNAOMBA MSAADA

TIMU ya soka ya New Hope FC ya watoto na vijana waishio mitaani wanatalajia kucheza michezo mbalimbali kwa ajili ya kuchangisha fedha za kituo chao kipya cha (New Hope Family Street Children-NFSC) kinachotalajiwa kufunguliwa Kigamboni.
Akiongea jijini Dar es Salaam , mratibu na afisauhusiano wa kituo hicho Andrew Chale alisema lengo ya michezo hiyo ambayo itakua ikichezwa kila jumamosi katika viwanja vya Gym khna ni kukusanya na kuchangisha fedha ambazo zitawasaidia watoto hao.
“Tunaomba jamii iliyoguswa na watoto hawa ambao wengi wao hali zao ni mbaya sana wanaitaji msaada wa haraka na kutimiza malengo yao ikiwemo ya kukaa pamoja katika nyumba maalum’ alisema Andrew.
Mchezo itakayochezwa siku hiyo ya jumamosi ni mpira wa miguu na riadha, ambapo itawakutanisha vijana na atoto mbalimbali wa vituo vya kulelea watoto wa waishio mazingira magumu na hatarishi.
Washiriki wengine watakaocheza michezo na watoto hao ni vijana kutoka kanisa la St.Columbus (St. Columbus Youth), Friends of Simba pamoja na watu mbalimbali watakao guswa na watoto hao.
NFSC wamekuwa wakikutana kila jumamosi katika viwanja hivyo kwa ajili ya kunywa chai kwa pamoja ambayo wanasaidiwa na wasanalia wema. “Wadau mutakao guswa na kilio chetu tunaomba msaada wa vitu vikiwemo vifaa vya michezo na maitaji mengine ikiwemo kujumuika na sisi hiyo jumamosi’ alimalizia Andrew.
Kwa upande wa Mwenyekiti Omary Rajabu alisema kuwa wanajisikia faraja kwa kupata nyumba ya kupanga iliyo na vyumba nane huko Kigamboni wakisubiri kulipiwa kodi ya mwaka Mil.1.2, fedha ambazo zimeaadiwa kulipwa na watu mbalimbali.
“Ombi letu kubwa sasa ni kuendelea kupata vitu vikiwemo vitu vya ndani kam vitanda,magodoro,nguo na vyombo vya kutumia pamoja na pesa kwa maitaji muhimu ya watoto hawa’ alisema Omary.
Kwa aliyegusw na umoja wa watoto hawa anaombwa kuwakilisha michango yake katika ofisi za gazeti la Tanzania Daima zilizopo katika jengo la Club Billicanas mtaa wa Mkwepu na kuonana na mhariri wa michezo, Deodatus Mkuchu ;0756090483 ama Andrew Chale 0719076376






No comments:

Post a Comment