Thursday, November 19, 2009

JAMANI PUNGUZENI ADHABU KWA WACHEZAJI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amelinyanyua juu kombe la FIFA la dunia wakati alipozindua rasmi ziara ya kombe hilo na kupiga nalo picha jioni hii kwenye uwanja wa taifa rais alipoingia kwenye kibanda maalum kilichojengwa kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuhifadhia kombe hilo akalibeba na kulinyanyua juu huku akilibusu kombe hilo, Rais Jakaya amewataka viongozi shirikisho la mpira wa miguu nchini Reodeger chila Tenga pamoja na kamati zake kufanya kazi ya kusimamia na kuinua kiwango na soka nchini badala ya kusimamia timu ya taifa tu na mapato ya milangoni kwani hawako TFF kwa ajili ya kujenga nyumba zao Binafsi bali wapo kwa ajili ya kuendeleza na kukuza soka nchini, Rais Jakaya amelaani kitendo cha shirikisho hilo kuwapa adhabu ya kuwafungia muda mrefu hadi miezi sita wachezaji na kusema hiyo ni kuwakomoa na kudidimiza vipaji vyao badala ya kuviendeleza , aliyeko kulia katika picha ni Hedi Hamer mwakilishi wa FIFA.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwasili kwenye uwanja wa taifa jioni hii ili kuzindua rasmi ziara ya kombe hilo nchini kushoto ni mke wake Mama Salma Kikwete na kulia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mh. Joel Bendera .



Na hili ndio pipa lililo beba kombe la dunia likiwa na nembo ya fifa kama unavyoweza kuliona kwenye picha


No comments:

Post a Comment