Wednesday, November 4, 2009

MISS UTALII INAPOCHUKA NAFASI

Kivumbi cha kumpata mrembo wa Fainali za Miss Utalii Ilala 2009 ni tarehe 6/11/2009 Ijumaa katika ukumbi wa Da’ West Park Inn Tabata, ambapo jumla ya Warembo 12 watapanda katika jukwaa kuchuana kuwania taji kwa musimu wa 2009/2010.Katika shindano hilo ambalo macho na masikio kwa wakazi wa Dar es Salaam limewatia wazimu kutokana na kutoelewa nani hataibua nderemo, Vifijo, na makelele kutokana na warembo wote kuwa katika hali ya Ushindani mkali ambapo kila mrembo amejigamba kuibuka na taji hilo kasha kubeba vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha thamani yake ikiwa ni milioni mbili .Warembo hao walioanza kambi kwa takribani mwezi mmoja katika Ukumbi wa Da’ West Park Inn-Tabata, waliweza kujifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na Utalii unaopatikana Tanzania ikiwemo Hifadhi za Utalii za Taifa, Vivutio vya Kitalii, pamoja na Maajabu ya Dunia yanayopatikana hapa Tanzania.Aidha katika shindano hilo, warembo hao wataonyesha Mavazi ya asili ya makabila mbalimbali ya Tanzania, watacheza ngoma kuonyesha utamaduni wa Mtanzania, Watavaa mavazi ya Kitanzania ya Kitalii, vazi la Ubunifu lililotengenezwa kwa maligafi za hapa Tanzania, pamoja na mengine mengi yanayohusiana na masuala ya Utamaduni wa Mtanzania.Warembo wanaowania taji la Miss Utalii Ilala 2009 ni pamoja na ,Tickey Lighton,Neema King’aka, Edna Endrew, Frola Nicholaus, Sheila Baamary, Janeth Samson, Nezia Gabriel, Roselina Sekwao, Jamida Abdu, Aghata Kilala, Tabus Thomas, na Shaymin Ntemena. Zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni kumi zitatolewa kwa washindi na washiriki, ikiwa ni pamoja na Fedha, na vifaa mbalimbali vyenye thamani mbalimbali, zitalolewa kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza kwa mujibu wa Waandaji wa shindano hilo ni thamani ya shilingi milioni 2, mshindi wa pili thamani ya million moja na laki mbili ,mshindi wa tatu thamani ya laki nane na , mshindi wa nne na tano, thamani ya laki tano na mshindi wa Kipaji (Talent) ni thamani ya laki saba na nusu na kifuta jasho kwa wote ni shilingi elfu thelathini na watapatiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki moja kila mmoja. Miss Utalii Ilala katika Msimu huu ilipata bahati ya Kuungwa Mkono kwa asilimia mia moja na Mkurugenzi wa Chicken Hut Tanzania ltd ya Mlimani City, Savannah Lounge- Paradise City Hotel iliyopo katika jingo la Benjamini Mkapa Tower-Posta Mpya, Chaga Bite iliyopo Kijitonyama, Kampala International University iliyopo Gongolamboto, pamoja na Ukumbi wa Da’ West Park Inn- Tabata.Wadhamini wengine waliojitokeza kuunga mkono ni wadau wa Shindano la Miss Utalii ikilinganishwa na miaka ya nyuma, ambapo baadhi ya watu mbalimbali wamejitokeza kusaidia ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Ulinzi na Usafirishaji ya Aurora, Kampuni ya Usafirishaji ya Mamaa Sakinma Trans, Mashujaa Pub, Kampuni ya Uongozaji Watalii na Usafirishaji Watalii ya Aucland Tours & Safari, Hotel ya Kisasa ya Grand Villa Hotel iliyopo Kijitonyama, Gym Ya kisasa ya Fitness Centre ya Chang’ombe (Oil Com), Saloon ya Kisasa ya Dage Saloon iliyopo Sinza, Kampuni ya Vifaa vya Umeme ya Vam General Suplay, Kampuni inayojishughulisha na Mti wa Maajabu Ya Mlonge(Mlonge by Makai Enterprises) na Wabunge wa jiji la Dar es Salaam Burudani mbalimbali zitapatikana katika kupamba Onyesho hilo ikiwa ni pamoja na Kundin la Muziki la Extra Bongo chini ya Ally Choki, Zia Musica,kundi la ngoma za asili Mfalme Bendi chini ya Costa Siboka zamani Mr Ginnes, na makundi mbalimbali ya muziki wa ngoma za asili, mwanamuziki wa kizazi kipya mtanzania anayeishi nchini afrika kusini Abubakari Ally (Kiboot) ambapo wote mnakaribishwa Da’ West Park Inn Tabata.

No comments:

Post a Comment