Friday, April 30, 2010

MAANDALIZI YA TAIFA CUP


Kaimu meneja mauzo wa TBL mikoa ya Kilimanjarona Tanga Edmund Rutaraka akimkabidhi kiasi cha shilingi milioni 1.5 katibu tawala msaidizi Hassani Bendeyeko kwa ajili ya maandalizi ya timu ya mkoa wa Kilimanjaro.huku zoezi hilo likishuhudiwa na makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro Darabu .m.Darabu na katibu wake Benedict Macha
Picha na Habari
Na Dixon Busagaga Moshi wa Globu ya Jamii, Moshi.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imekabidhi kiasi cha shilingi milioni 1.5 timu ya mkoa wa Kilimanjaro “Kilimanjaro Worrios kwa kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya taifa cup.
Fedha hizo zilikabidhiwa jana kwa katibu tawala msaidizi Huduma na miundombinu Hassani Bendeyeko kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia alikabidhi fedha hizo kwa viongozi wa chama cha soka mkoa KRFA.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo kaimu meneja mauzo mikoa ya Kilimanjaro na Tanga Edmund Rutaraka alisema kampuni hiyo imetoa kiasi hicho cha fedha ikiwa ni sehemu ya udhamini pamoja na kuwapa motisha wachezaji.
“Mh katibu tawala msaidizi kwa niaba ya mkuu wa mkoa ,kama lilivyo jina la mashindano lenyewe Kilimanjaro Taifa cup na mkoa wetu ni Kilimanjaro ,tukasema ni vyema tulete pesa hizi ili ziweze kusaidia timu katika maandalizi na wachezaji waweze kupata motisha”alisema Rutaraka. Alisema kampuni hiyo itaendelea kusaidia maendeleo ya soka ikiwa ni pamoja na kuwapa ari wachezaji ili waweze kushiriki mashindano mbalimbali kwa kiwango cha juu.
Akizungumzia zawadi za mwaka huu Rutaraka alisema mshindi wa kwanza mwaka huu atapata shilingi milioni 30 ,wa pili miliono 20 wa tatu milioni 10 na wanne 5 huku akiwataka vijana wajitume ili waweze kupata zawadi moja kati ya hizo.
Naye Katibu tawala msaidizi Bendeyeko aliipongeza TBL kwa jitihada zao na kutoa mwito kwa makampuni mbalimbali, mashirika na watu binafsi kujitokeza kuisaidia timu ya soka ya mkoa wa Kilimanjaro ili iweze kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Bendeyeko alisema kuandaa michezo kama ya mashindano ya Kombe la Taifa ni gharama kubwa na kutokana na hilo TBL inapaswa kupongezwa kwa hilo na kutoa mwito kwa kampuni nyingine kuiga mfano huo ili kuinua michezo mingine badala ya soka pekee Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro Darabu M Darabu alisema kiasi hicho cha fedha kitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa huku akiwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuisadia timu hiyo.

kwa HISANI YA issamichuzi.blogspot.com/


No comments:

Post a Comment