Saturday, April 24, 2010

MUZIKI WETU

Oscar Nyerere kusindikiza.Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini katika muziki wa Dansi, Ramadhani Masanja(Banza Stone) siku ya Alhamisi ya tarehe 6 may 2010 anatarajia kuzikoga nyoyo za wapenzi wa muziki katika kitongoji cha Sinza wakati hatakapokuwa mgeni mwalikwa kwenye onyesho la Bendi Mpya naya kisasa ya Mashujaa Musica ambayo itakuwa mara yake ya kwanza ikiwa na Elyston Angai ambaye ni mkali wa zama za Diamond Sound wana kibindankoi, kufanya onyesho ndani ya ukumbi huo.

Wakizungumzia maandalizi hayo, waratibu wa Onyesho hilo, Aloyce Java kwa kushirikiana na Mussa Mwidadi, Johakimu Rasta, walisema kuwa shoo hiyo itaanza saa tatu Usiku ambapo itasindikizwa na msanii nyota wa vichekesho na mwenye uwezo wa kuigiza sauti mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za Viongozi akiwemo Baba wa Taifa-Mwalimu Julius Kambarage Nyerere maarufu kwa jina la Osca Nyerere.

Na kwamba wapenzi wote wa burudani kitongoji cha Sinza fikeni ili kuona Mashujaa Musica wanavoonyesha Ushujaa wao kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Vatcan Hoteli ambapo Banza pamoja na wanamuziki hao watapanda jukwaa moja katika kuwapa raha mashabiki ikiwa ni pamoja na kupata Sebene kali zote za bendi hiyo.

“tumeandaa shoo hiyo ili kuwafanya wakazi wa Sinza na wote watakaofika kupata raha, nasema raha kutokana na jinsi tulivyoandaa, kwani katika kunogesha tumeamua kumuita Banza Stone, unajua tena wewe mwenyewe ndugu mwandishi, Banza akiwa sehemu ama naweza kusema sauti yake, ukichanganya na vitu vya Elystoni Angai, kama unakumbuka wakati ule Elyston alipokuwa Diamond Sound wanakibindankoi, bila shaka raha siku hiyo itakuwa aina kikomo, pamoja na kwamba itakuwa mara ya kwanza kuwakutanisha Mashujaa nan Banza kufanya onyesho Sinza, nina imani kubwa shoo hiyo itakuwa ya kuvutia”alisema Mussa Mwidadi

Baadhi ya wanamuziki wa Mashujaa Musica wanaotarajia kuwasha moto siku hiyo ni pamoja na Ibrahim Milinda Nyeusi, Jadol Fidifosi, Zidane(Sauti ya Nyati), Ngosha Mwanamasanja, Pasia Budansi,Raja Rada,Masoud Usb, Amosi Mkono wa Nabii, Baba Isaya, Despino Malaika, Komba Bess, Komputer, Sele Kadanse, na kuongeza kuwa wanenguaji wote mahiri watakuwapo ikiwa ni pamoja na Sharony Mapozy, Mariam Leila Pee, Merisa Ngwasuma, Pendo Bonzo, Salha Sarehe, Sarafina Shotii, Rose Masaki, na Flora Bambucha. kwa kiingilio cha shilingi elfu tano tu kila mmoja .

No comments:

Post a Comment