BINGWA wa Dunia wa uzito wa middle anayeshikilia taji ya ICB, Francis Cheka jana usiku alifanikiwa kuutetea mkanda wake baada ya kumtwanga bingwa wa Dunia wa Kickboxer, Japhet Kaseba kwa TKO.
Cheka anashikilia mkanda huo tangu mwaka jana baada ya kumtwanga kwa KO Hassan Matumla katika raundi ya 10 ya mchezo wao.
Pambano hilo lililoshihudiwa na mamia ya wapenzi wa mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Kaseba ambaye alionesha ukomavu baada ya kuweza kumihili ngumi nzito za Cheka katika raundi nane zilizopita lakini raundi yatisa alishindwa kuhimili kishindo hicho baada ya kukubali kwenda chini baada ya kutwishwa ngumi nzito lililompereka kwenye kamba na kuanguka chini.
Cheka ambaye alitamba kummaliza Kaseba baada ya raundi ya sita alifanikiwa kufanya hivyo katika raundi hiyo ambapo alimpiga mpinzani wake ngumu ya kidevu na kujikuta akiwa chini.
Baada ya ngumi hiyo mwamuzi wa mchezaji huo, Antony Lutta alisimamisha pambano na kumwesabia na Kaseba alikuwa tayari kuendelea na pambano hilo.
Cheka kwa kuwa alikuwa tayari kwa kummaliza Kaseba alimvamia na kumsukuma kwa ngumi ambayo ilimfanya Kaseba aende tena chini lakini hata mwamuzi aliposimamisha mchezo Cheka hakusikia na kuendelea kumshambulia.Hali ya kushambuliwa Kaseba bila kikomo ilimshinda msaidizi wake na kuamua kuingia ulingoni na kumbeba Cheka na kumtupa nje ya ulingoni.
Baada ya tukio hilo pambano lilivulugwa kutokana na fujo zilizokea pande mbili za mashabiki wa mabondia hayo.
Kutokana na vulugu hizo mwamuzi wa pambano hilo aliamua kumpa ubingwa Cheka kwa kuwa kitendo kilichofanywa na msaidizi wa Kaseba ni sawa na kutupa taulo kumwokoa bondia wake.Kwa kipigo alichopokea Kaseba kinadhihirisha kuwa bondia huyo kutoka mkoani Morogoro kuwa bado hana mpinzani katika ramani ya mchezo huo kwa sasa baada ya kuwachapa ndugu wawili, Hassan na Rashid Matumla.Cheka alianza kutawala mpambano huo tangu raundi ya nne kutokana na kupata nafasi ya kumshambulia mpinzani wake kutokana na mtindo wake wa kuzuia zaidi.
Mpambano huo ulitanguliwa na mapambano ya utangulizi ambapo Mada Maugo alimtwanga wa KO Kanda Kabongo katika raundi ya pili, Habibu Pengo alimchapa kwa KO raundi ya kwanza Adrias Charles na Francis Suba alipigwa kwa pointi na Antony Mwakapalila.
Mapambano mengine ni Lesekelo Daud alimshinda kwa pointi Baraka Nuhu, Charles Mashari alishinda kwa pointi Omary Ramadhani, Habibu Mganda alimchapa kwa pointi Sadick Momba na mchezo pekee wa wasichana kati ya Pendo Njau aliyemtwanga kwa pointi Flora Paul.Katika michezo ya Kickboxing Mrisho Van Damme alimtwanga kwa KO Mrisho Jumanne, Emmanuel Shija alimchapa kwa KO raundi ya pili Mohamed Kidevu na Shukuru Samata alishinda kwa KO raundi ya pili Said Kuchi.
Mpambano huo wa ubingwa kati ya Cheka na Kaseba ulidhaminiwa na kampuni ya Business Times Ltd wachapishaji wa magazeti ya Majira, Business Times, Dar Leo na gazeti la michezo la Spoti Starehe linalokuwa mtaani kila Alhamisi na Jumapili na Zain.
Bondia Mada Maugo wa Tanzania akitupa konde la kushoto kwa mpinzani wake Kand Kabongo wa Zaire wakati wa pambano lao la kirafiki lililofanyika Dar es salaam juzi Maugo alishinda kwa KO ya raundi ya pili.(Picha na Rajabu Mhamila)
No comments:
Post a Comment