JIJI la Mwanza limeendelea kutesa katika fani ya urembo baada ya juzi usiku mrembo Miriam Gerald kufanikiwa kutwaa taji Miss Tanzania 2009, shindano lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Mwanza imewatesa warembo kutoka mikoa ya Tanzania baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa miaka miwili mfufulizo baada ya mwaka jana taji hilo kunyakuliwa na Nasreem Karimu naye kutoka jiji hilo.
Miriam ambaye ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, pia jana alifanikiwa kuondoka na Suzuki Vitara mpya.Mbali na taji hilo pia Miriam ndio Mrembo mwenye mwonekano mzuri katika picha baada ya kunyakua taji la Redd's Photogenic na kujinyakulia kitita cha sh. milioni moja na mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa balozi za kinywaji cha Redd's.
Nyota ya Miriam ilianza kung'ara tangu mapema kwani kila alipopanda jukwaani katika mavazi mbali mashabiki walimshangilia kwa kelele kutokana na urembo wake.
Miriam alipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki baada ya kuamua kujibu swali aliloulizwa kwa kiswahili kwa kuwa ndio lugha yake ya Taifa, hali iliyoamsha ndelemo na vifijo ukumbini hapo.Nafasi ya pili ilikwenda kwa mrembo kutoka Ukanda wa Vyuo Vikuu, Beatrice Lukindo wakati mrembo aliyeiwakilisha kanda ya Ilala, Judith William alishika nafasi ya tatu.
Nafasi ya nne ilinyakuliwa na mrembo kutoka Silvya Shally kutoka Ilala na nafasi ya tano ilikwenda kwa Sia Ndasoki aliyeiwakilisha kanda ya Temeke.
Warembo 10 kati ya 29 waliofanikiwa kuingia katika hatua ya 10 bora ni Miriam Gerald, Beatrice Lukindo, Julieth William, Silvya Shally, Sia Ndasoki, Ivony Birigwa, Susan Emmanuel, Gladys Shao na Evelyne Gamasa.
Warembo wengine ambao walifanikiwa ktwaa mataji mengine ni Tory Oscar aliyetwaa taji la mrtembo mwenye kipaji na kujinyakulia sh. 500,000 kutoka hoteli ya Giraffe Ocean View.
Mwingine ni Judith William ambaye ametwaa taji la kuwa balozi wa Utalii wa ndani na kujinyakulia zawadi zenye thamani ya sh. milioni 3.3 kutoka kwa Bodi ya Utalii Tanzania.Mrembo huo amejinyakulia compyuta ndogo (laptop) mpya pamoja na pesa taslimu sh. 1,100,000.
Warembo wengine walioshiriki shindano hilo ni Glory Chuwa (Tanga), Jackline Nitwa (Dodoma), Shany Anthony (Temeke), Wagala Shungu (Higher Learning Institute).
Wengine ni Julieth Willium (Ilala), Sabina Bododi (Mara), Stellah Chidodo (Singida Kanda ya Kati), Ester Gao (Higher Learning Institute), Doris Deogratius (Higher Learning Institute), Sandra Malebeka (Kinondoni), Stella Solomoni (Temeke) na Mary Lucas (Southern Hinglands).Pia wapo Aloycia Innocent (Kinondoni), Precious Donald (Pwani), Maria Daniel (Arusha), Gloria Mayowa (Lindi), Lulu Ibrahimu (Kinondoni), Glory Willium (Ilala), Catherine Letara (Southern Hinglands) na Mary Joseph (Mara).
Shindano hilo ambalo lilifurika watu wengi lilipambwa na burudani mbalimbali za muziki wa asili ikiwa pamoja na muziki wa kizazi kipya kutoka kwa wasanii maarufu nchini pamoja na Uganda.
No comments:
Post a Comment