Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda akiwa na Balozi Mwanaidi Maajar, Katibu Mkuu wa TA Hassan kushoto na kulia Mwenyekiti wa TA John Lusingo.
Na Ally Muhidin.
Waziri Mkuu Akutana na Jumuiya za Watanzania, London
Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amekutana na viongozi wa jumuiya mbalimbali za Watanzania waishio nje ya nchi.
Mh. Pinda amekutanna viongozi hao katika ofisi za ubalozi wa Tanzania zilizopo London, Uingereza kujadiliana nao kwa jinsi gani wameweza kuiletea maendeleo katika nchi yao.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Bi. Mwanaidi Maajar alimkaribisha Mh. Pinda na kutambulisha kwa maafisa wa Ubalozi pamoja na Kiongozi wa Jumuiya za Watanzania Bw. John Lusingu ambaye nae aliitambulisha Jumuiya nzima kwa Mh. Pinda.
Mwenyekiti wa TA nchi Uingereza Bw. John Lusingu alimueleza Waziri Mkuu mikakati na mipango ambayo Jumuiya hiyo inafanya kuweza kuwasaidia Watanzania waishio Nje ya nchi pamoja na wale waliopo nyumbani.
Mikatika hiyo ni kuhusu suala zima la Michezo, Kilimo, Usafiri, Habari, mfumo mzima wa huduma za mazishi na matatizo ya Watanzania yanayowakabili katika masuala mbalimbali.
Mh. Pinda alisema serikali ipo tayari kuwasaidia Watanzania wote watakaojitokeza kuelezea matatizo yao na hivi sasa serikali inaangalia wananchi wenye hali duni ili kuweza kuboresha maisha ya wananchi hoa.
Serikali imevipa kimaumbele Elimu, Maji, Bandari, Barabara, na Umeme na inaangalia jinsi gani itakavyoweza kuboresha huduma hizo. Alisema Mh. Pinda
Mh. Pinda alimsifia Balozi Maajar kwa jinsi gani ameweza kuwasaidia Watanzania wawe na Jumuiya na mchango wake mkubwa katika masuala mbalimbali ya kuwasaidia Watanzania waishio Uingereza.
Mh. Pinda ameichangia Jumuiya hiyo kiasi cha £2000 na kuahidi kuwa serikali itaangalia jinsi gani itakavyoweza kuwasadia katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Balozi Maajar alimshukuru Mh. Pinda kwa mchango wake wa kuja kuangalia maendeleo ya Watanzania na kuichangia Jumuiya hiyo.
Habari hii ni kwa hisani ya Ally Muhidin
Kwa picha Zaidi bofya hapa
http://www.tz-one.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment