Friday, August 21, 2009

Benedicto Mtungirehi alejeshwa Uanachama TLP

Katibu mkuu wa chama TLP Jonh j Komba akisoma barua ya kuludishwa uanachama Bw Benedicto Mtungirehi aliyeshika kalamu mwingine ni Rajab Hamad Tao ambye hayupo pichani katika makao makuu ya chama cha TLP Manzese Argentina
Chama Tanzania labour party kimemrejeshea uanachama Bw Benedict Mtungirehi baada ya kulizika kuwa amejirekebisha makosa yake ambayo aliyafanya. akitanabaisha makosa hayo Katibu mkuu wa chama hicho taifa bw John j Komba alisema kuwa kosa alilofanya Mtungirehi ni kutoa taarifa kwa msajili wa vyama vya siasa baada ya kutoa taarifa katika kikao cha chama hicho kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ibara ya 18.9(e) kinasema kuwa matatizo ya ndani ya chama yatatuliwa ndani vikao vikuu vya Chama na sio nje ya Chama aidha kwa upande wake bw mtungirehi amesema kuwa ni wakati mzuri sasa kujenga upya chama na kuacha migogoro ambayo haina msingi na kuwa chama ndio chenye uwezo wa kumtoa au kumrudisha mwanachama uanachama wake.

No comments:

Post a Comment