Monday, April 26, 2010

Kashfa katika kriketi India


 
Mwenyekiti wa baraza la kriketi anakabiliana na madai ya rushwa

Baraza linaoloyasimamia mashindano yanayoingiza senti nyingi zaidi ulimwenguni, ligi ya Premier ya India, limemchagua mwenyekiti wa muda, kufuatia mkutano wa dharura kuzungumzia juu ya madai ya mwenyekiti Lalit Modi kuhusishwa na rushwa na uwekezaji katika biashara zisizo halali.

Bodi hiyo ya kriketi jana usiku ilimsimamisha kazi Bw Modi, dakika chache tu baada ya fainali ya kukamilisha msimu huu mjini Mumbai.

Ligi hiyo, ambayo wengi huifikiria kwamba huchangia katika kustawisha na kuimarisha uchumi wa India, huwashirikisha baadhi ya wachezaji bora zaidi duniani, na ambao huzichezea timu zinazomilikiwa na matajiri wakubwa na wacheza filamu mashuhuri nchini India.

Mwandishi wa BBC anaelezea kwamba kwa ligi hiyo kuunganisha kriketi na burudani, ni jambo ambalo limeyafanya mashindano hayo kupata umaarufu mkubwa duniani.
 



No comments:

Post a Comment