Friday, April 23, 2010
RUBGY KURUSHWA JUU NA PRECISION AIRWAY
Meneja Masoko wa kampuni ya Precision Air, Emillian Rwejuna wa pili kutoka (kushoto) akikabidhi fulana pamoja na mipira kwa Makamu wa Rais wa Muungano wa vyama vya mchezo wa Rugby, Chris Hatty (kulia) ikiwa ni sehemu ya udhamini kwa timu ya taifa ya mchezo huo inayokwenda leo mjini Arusha kushiriki michuano ya kimataifa kwa nchi za Afrika Mashariki. Katikati ni Rais wa Muungano wa vyama vya mchezo huo, kulia ni Tinus Aucamp makamu mwenyekiti wa chama cha Rugby na mwisho kushoto ni Ibrahim Bukenya Meneja mauzo. Kampuni hiyo pia ilitoa tiketi za ndege kwa ajili ya wachezaji pamoja na viongozi watakaoambatana na timu hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar.
Kwa hisani ya fullshangwe.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment