Monday, July 19, 2010

NETBALL VP MPO AU MMELALA


Timu Kumi na sita za mchezo wa Pete zinatarajia kushiriki michuano ya klabu bingwa taifa itakayotimua vumbi jijini DSM wiki hii.

Katibu Msaidizi wa chama cha mpira wa pete Tanzania CHANETA, ROSE MKISI amesema mashindano hayo ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo.

Aidha CHANETA imezishusha daraja timu ya Uhamiaji ya DSM na Ras ya Mtwara kutokana na kushindwa kutoa taarifa juu ya ushiriki wa michuano hiyo.

Michuano hiyo pia aitasaidia kupata wachezaji bora kwa ajili ya kuunda kikosi cha timu ya taifa kinachokabiliwa na mashindano ya kimataifa yakiwemo ya Afrika na Dunia hapo baadaye mwaka huu..

janejohn.blogspot.com/





No comments:

Post a Comment